Tuesday, 9 August 2016

Elimu bure yasaidia watoto waliokuwa wanajihusisha na uchimbaji wa madini

Na Ghati Mahenye 
Watoto katika vijiji vinavyozunguka mgodi wasaidiwa na mchakato wa elimu bure ulioanzishwa na Rais John Pombe Magufuli. Maneno hayo yamesemwa na wanakijiji wa Genkuru na kueleza ni jinsi gani elimu hiyo imesaidia Watoto hao wengi waliokuwa wanajihusisha na uchimbaji mdogo wa madini wamerudi shule kwani kwa sasa ada za shule zimefutwa na imepuguza kikwazo kikubwa kilichokuwa kinawafanya wasiend shule, hivyo watoto hao wameona hamna haja ya kuvamia mgodi huo. Pia wameeleza ni kwa jinsi gani elimu bure imewasaidia na kuwaokoa katika madhara makubwa waliyokuwa wakiyapata wawapo mgodini kama vile; kukosa elimu, kufanya kazi ngumu machimboni na hata kupata kipato kidogo ambacho hakikutosha kukidhi mahitaji yao. Wanajamii kwa upande mwingine, wamelipokea hili swala kwa furaha na wameomba viongozi wa viijiji watilie mkazo watoto wote warudi shule kwa kuandaa mikutano ya hadhara ya kuhamasisha wazazi kuwasomesha watoto wao kwani ndo taifa la kesho. Elimu bure imeonekana kuwa na mchango mkubwa katika vijiji vilivyo kuwa vinauzunguka mgodi kwani wameondokana na jamii ambayo watu hawasomi na sasa kuwekeza kwenye elimu. Kwa kuhitimisha, wanakijiji wamesisitiza nijukumu la kuwasaidia watoto hao na kuhakikisha wanamaliza masomo hayo bila vikwazo vyote.

No comments:

Post a Comment