Na John Honga Wambura
Kauli mbiu ya Rais John Pombe Magufuli ya ‘HAPA KAZI TU’ imesaidia kupunguza idadi ya vijana wanaojihusisha na shughuli za uvamizi wa mgodi uliopo Mara Kaskazini. Hili ni baada ya wanachama wa Vilabu vya Umoja chini ya usimamizi wa shirika la Search for Common Ground kufanya utafiti kwa njia ya mahojiano kati ya wanachama hao na wanakijiji wa kijiji cha Genkuru mwezi wa sita mwaka huu na kubaini kuwa vijana wengi kwa sasa wameacha kujihusisha na shughuli za uvamizi wa migodi inayomilikiwa na mwekezaji wa ACACIA iliyopo Mara Kaskazini.
Lakini pia, imeelezwa kuwashughuli hizo zilikuwa zikifanyika kwa lengo la kujipatia kipato ili kujikimu katika maisha yao
Pia katika mahojiano hayo wanakijiji wengi wamekubali kuwa walishawahi kujihusisha na shughuli za uvamizi lakini pia kuna wachache kati yao ambao hawajawahi kufanya shughuli za uvamizi wa migodi.
Hivyo basi, katika mahojiano juu ya umuhimu wa kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ katika kupunguza uvamizi wa mgodi wengi waliweza kutoa maoni yao kama ifuatavyo:
Kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ imesaidia kwa sababu, vijana siku hizi hawachagui kazi ya kufanya kama awali ambapo vijana wengi walikuwa wanaona kazi muhimu ni uchimbaji wa madini katika eneo la mgodi. Hivyo, kauli hiyo imesaidia sana kupunguza vijana na kufanya vijana wengi kuwa na mwamko wa kazi.
Kwa upande mwingine, kauli mbiu ya Rais Magufuli ya ‘Hapa Kazi Tu’ imesaidia kupunguza idadi ya vijana wanaojihusisha na shughuli za uvamizi wa mgodi kwasababu imepelekea vijana kujiajiri wenyewe katika kazi nyinginezo ambazo ni kama kilimo, ufugaji na biashara ndogo ndogo pia ameeleza kuwa pamoja na kauli mbiu ya Rais, pia idadi hii imepunguzwa na uhaba wa madini kuliko hapo awali ambapo yalikuwa yana mwagwa kwa wingi.
Kwa kuzingatia umuhimu wa kuli mbiu ya Rais Magufuli vijana wengi wavamizi wa mgodi wamepungua sana kwa kuwa polisi wamekuwa makini na kazi yao na kuacha uzembe.
Hata hivyo, pamoja na kuwa wanakijiji wengi walikubali kuwa kauli mbiu ya Rais Magufuli imesaidia kupunguza idadi ya wavamizi mgodini ila kuna wanakijiji wengi waliokuwa na mtizamo tofauti wakisema yafuatayo:
Ni jambo lisilo na uhakika kuwa kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ imesaidia vijana wanaojihusisha na shughuli za uvamizi wa mgodi kwasababu ni kweli kwamba, kwa sasa idadi hiyo ya vijana imepungua lakini ni kutokana na ulinzi kuwa makini pamoja na vijana wengi kukosa madini
wanapokuwa wanaenda mgodini kwani kwa sasa idadi kubwa ya madini yamepungua kwakipidi hiki cha sasa si kama ilivyokuwa hapo awali.
Katika mahojiano haya na wanakijiji wamependekeza ya kuwa ili kauli mbiu ya Rais Magufuli iweze kufanikiwa kupunguza idadi ya vijana wanojihusisha na uvamizi wa migodi nimuhimu vijana wapewe elimu ya ujasiriamali na pia nafasi za ajira na hata mikopo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Kwa kuhitimisha, kwa sasa wakazi wa vijiji wanaozunguka mgodi wa Mara Kaskazini wameanza kuonyesha mabadiliko kwa kuanza kufanya kazi tofauti na uvamizi wa mgodi ikiwa ni sehemu ya kuheshimu kauli mbiu ya Rais Magufuli ya ‘Hapa Kazi Tu’.
No comments:
Post a Comment