Tuesday, 9 August 2016

Vijana wa Mara Kaskazini waaswa kujishughulisha na kuacha utegezi wa mgodi

 Na Matinde Kesonko
Vijana katika eneo la Mara Kaskazini waombwa kuwa wabunifu wa miradi mbalimbali ya kujiendeleza kimaisha na kuacha utegemezi wa migodi, maneno haya yamesemwa na Afisa Mtendaji wa kijiji cha Msege baada ya kukutana na vijana kutoka Sauti ya Mara Kaskazini.
Mtendaji huya ameyasema haya baada ya vijana waliokuwa waanajihusisha na uvamizi wa mgodi wa Mara Kaskazini kupungua na wengine kuacha huku wengi wao wakishinda vijiweni bila kufanya mambo ya msingi.
Pia vijana hao wameombwa kufanya shughuli ndogo ndogo za kukidhi mahitaji yao binafsi. Shughuli hizo ni kama ufugaji, kilimo na ujasiriamali ili waweze kuondokana na umaskini na vitendo viovu wanavyofanya kama uvutaji bangi na kushinda vijiweni wakipiga porojo.
Vilevile vijana hao wameomba kutengewa maeneo na serikali iliwaweze kufanya shughuli za uzalishaji iliwaweze kuondokana na umaskini, vijana hawa wametoa maoni haya na kusisitiza kwamba kazi ya uvamizi wa mgodi ni ngumu na wanakumbana na matatizo mengi kama ulemavu, vifo na hata migogoro ya wenyewe kwa wenyewe.
Hivyo basi serikali imeombwa kutilia maanani hili swala kwani vijana wengi hawana ajira katika eneo la Mara Kaskazini. Vijana hawa wameomba kupewa mikopo mbalimbali waunde vikundi mbalimbali ya ili waweze kujiendeleza.
Kwa kuhitimisha, ni dhahiri vijana wa Mara Kaskazini wanahitaji msaada wa kimawazo, kifikra na kifedha kutoka kwa wadau mbalimbali kutoka asasi binafsi na serikali kwa ujumla.

1 comment:

  1. that is good ......endeleeni hivyo hivyo katika utoaji wa elimu

    ReplyDelete